Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la upasuaji na Dk.Sylvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,Daktari Kabutura  alimueleza Katibu Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika kituo hicho,na pia kutokamilika kwa jengo kubwa la huduma za upasuaji na huduma nyingine zaidi ya mwaka,jambo ambalo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana hakufurahishwa nalo,kwani kumekuwepo na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi wilayani humo kwa ukosefu wa huduma mbalimbali za afya kwa Wananchi kufuatia kutokamilika kwa jengo hilo na miradi mingine mbalimbali ya zahanati iliyosababishwa na Mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi wa miradi hiyo,kwa wakati.
  Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto),kati Dk.Sylvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye wakimsikiliza.

Akitolea Ufafanuzi zaidi kuhusua suala hilo,Mbunge wa Jimbo la Sikonge,Mh Said Mkumba ameeleza kuwa,Mkandarasi wa ujenzi wa vituo hivyo vya Afya,ameshindwa kumaliza kazi kwa wakati,wakati mkataba ulianza mnamo 28/10/2009 na ulipaswa kumalizika 2/5/2011,lakini mpaka sasa vituo hivyo na zahanati havijakamilika,jambo ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo katika suala zima la Afya wilayani humo.

Mh.Mkumba alizidi kubainisha kuwa kupitia Mradi wa Kupunguza vifo kwa akina mama Support to Martenal Mortality Project Reduction (SMMRP).Jumla ya vituo saba vya kutolea huduma za Afya Wilayani Sikonge vilitakiwa kujengwa,vikiwa ni Kipili,Kitumbi,Tumbili,Pangale,Kitunda,Mazinge na Kisanga,ambapo jumla ya shilingi bilioni 2,051,723,850 zimelipwa kwa mkadarasi huyo,lakin hata hivyo kazi hiyo haijakamilika mpaka sasa. 
Wananchi wa  kijiji cha Lukula,katata ya Kitunda wakimsikiliza  Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba,wakati akielezea mambo mbalimbali waliyoyatekeleza kupitia chama chake cha CCM,na pia akionesha ni namna gani amekuwa akikerwa na kunyonywa kwa Wakulima wa zao la Tumbaku,wilayani humo kupitia Vyama vya Ushirika,ambavyo vimefuja kiasi kikubwa cha fedha na kuwaacha wakulima hao katika sintofahamu huku maisha yao yakiendelea kuwa duni siku hadi siku.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mgambo kitongoji cha Lukula  kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkani Tabora ambapo aliwaomba radhi wakulima wa Tumbaku kwa kadhia waliyo nayo kutokana na kunyonywa na kutopata haki zao za malipo kwa miaka 3.Kinana aliongeza kuwa pamoja na kuwaomba radhi wakulima hao wa Tumbaku,amesema waruhusiwa kuuza tumbaku yao wanapotaka,kwa sababu vyama vya ushirika vya msingi vimekuwa vikiwadhulumu kwa kiasi kikubwa wakulima hao.Aidha Kinana ameahidi suala hilo la dhuluma kwa Wakulima wa tumbaku na sualal la Zahanati kuyafikisha kwa Dkt.Rais Jakaya Kikwete.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 Mkulima wa zao la Tumbaku Lameck Mnyama akitoa ushuhuda na malalamiko ya wakulima wa zao hilo,kwa namna ambavyo vyama vya ushiriki  vimekuwa vikiwaibia na kushindwa kuwalipa fedha zao kwa wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikazia jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa na  Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye wakimsikiliza mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji  cha Lukula katika kata ya Kitunda,wilayani Sikonge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...