Madiwani wa Chama cha CUF,wilayani Urambo wakimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.Shoto ni Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda na kati ni Diwani wa CUF,Kata ya Usoke,Mh.Kadada Mohamed,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya elimu,afya na maji katika halmashauri ya Urambo mkoani Tabora.Pichani nyuma ya Kinana ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akifurahia jambo.
Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda akimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh.Samwel Sitta mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Wilayani Urambo mapema leo.
 Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta akimkaribisha katika jimbo lake Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo.
 Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta,Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa,Mh.Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Uyumbu,katika kata ya Uyumbu wilayani Urambo mkoani Tabora.

Picha na Michuzijr-Urambo Tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...