Na Geofrey Tengeneza
Onesho la Kimataifa la Utalii la Tanzania lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo (S!TE) linaroratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB na litakalokuwa likifanyika kila mwaka mwezi Oktoba katika eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam limetambulishwa rasmi kwa wadau mbalimbali waliohudhuria maonesho ya Kimatatifa ya Utalii ya INDABA huko Durban Afrika Kusini.
Akizungumza wakati wa kutambulisha onesho hilo, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mh. Radhia Msuya amewaambia washiriki wa INDABA kuwa onesho hilo litakuwa likifanyika kila mwaka na kwa kuanzia mwaka huu litafanyika tarehe 1 -4 Oktoba.
Amesema kuwa S!TE linatarajiwa kuwa onesho la pilii kwa ukubwa barani Afrika baada ya lile la INDABA na amewakaribisha wadau na makampuni yote yaliyoshiriki maonesho ya INDABA kushiriki pia onesho hilo la S!TE.
Maonesho ya INDABA hufanyika Durban Afrika Kusini kila mwaka mwezi Mei ambapo mwaka huu yalifanyika kuanzia tarehe 10-12 Mei na waoneshaji kutoka Tanzania uliongozwa na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Profesa Isaya Jairo. Jumla ya makampuni 41 kutoka Tanzania yalishiriki katika maonesho hayo.
Baadhi ya washiriki wa taasisi za Serikali
katika Banda la Tanzania wakati wa maonesho ya INDABA Afrka Kusini.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji na Mkurugenzi wa
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi akitoa maelezo
kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la
Tanzania katika maonesho ya INDABA huko Durban Afrika Kusini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...