Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimpokea kwa furaha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Ahmet Dovutoglu ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki.
|
Mhe. Membe akiwa ameongozana na Mhe. Dovutoglu mara baada ya kumpokea wakielekea katika Hoteli ya Hyatt Regency kwa ajili ya mazungumzo rasmi.
|
Mhe. Membe na Mhe. Dovutoglu wakiwa na Wajumbe waliofuatana nao wakati wa mazungumzo rasmi.
|
Mhe. Membe kwa pamoja na Mhe. Dovutoglu wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuangalia namna Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linaweza kushirikiana na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines)
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...