Kozi ya ukocha wa mpira wa miguu ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyokuwa ianze kesho (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa itafanyika mwezi ujao.


Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na kuendesha kozi hiyo itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.

Tarehe rasmi ya kuanza kozi hiyo itatangazwa wiki ijayo. Mwezi uliopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya leseni B iliyoshirikisha makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...