Meya
wa Manipaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewataka wananchi wa Manispaa
yake na nchini kote kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza ili
kupunguza tatizo la watoto wa mitaani na mayatima ambao wamekuwa
wakiongezeka kila siku jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa futari aliyoiandaa kwa wananchi wa Manispaa yake, viongozi wa
Kiserikali na kidini, Dar es Salaam juzi Meya huyo alisema kuwa
Manispaa yake ni kubwa na hivyo endapo watu watachukua maamuzi ya
kusaidia watoto hao basi tatizo hilo litakuwa limepungua kwa kiasi
kikubwa katika Manispaa hiyo na jijini kwa ujumla.
“Wito
wangu kwenu tuwasaidie watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira
magumu katika Manispaa yetu ili kuondoa tatizo hili la watoto wanaozagaa
mitaani kwani nao wana haki kama walivyo watoto wengine wenye wazazi na
wanaoishi kwenye mazingira mazuri. Nazungumza hili kwa kuwa hili ni
tatizo sugu katika Manispaa yetu.” Alisema.
Aidha
aliwahakikishia wananchi hao kuwa Manispaa itaendelea kufanya kila
inachoweza kuhakikisha inaboresha hali ya maisha ya wananchi wake bila
kujali itikadi za kisiasa wala kidini ili kuondoa umasikini kwa wananchi
hao. Pia alisema Manispaa itaendelea kusimamia kampeni yake ya kuweka
mazingira safi ya Manispaa kwa kuhakikisha inatimiza malengo yake
iliyojiwekea.
“Niseme
kuwa sisi (Manispaa) ndio tunaoondoa taka kwa asilimia 75 hapa jijini,
nawapongeza Madiwani wangu kwa kusimamia vema kampeni mbalimbali
tunazozianzisha katika Halmashauri yetu.” Alisema
Kwa
upande wake Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Saluma
aliwahimiza waumini wa dini ya Kiislam kuzidisha ibada katika kumi hili
la mwisho la mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kusema kuwa endapo
muumini atakutwa na usiku wa lailatul qadir basi ni sawa na kufunga
miezi 1000 ambayo ni sawa na miaka 83.
Shehe
wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda (mbele) akiowaongoza
waumini katika swala ya Magharibi, kabla ya kupata futari iliyoandaliwa
na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kwa wananchi wa Manispaa
yake, viongzoi wa kiserikali na kidini, Dar es Salaam jana. Kutoka
kulia (mstari wa mbele) ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaabn Bin
Simba, Imam wa Msikiti wa Alfarouq, Mwita Kambi, Shehe wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Alhad Mussa Salum, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda,
viongozi mbalimbali wa dini na wa kiserikali.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akiwaongoza wageni
mbalimbali kupakua futari aliyoindaa kwa wananchi wa Manispaa yake,
viongozi wa kiserikali na wa kidini, Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Shehe wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto0 akipata
futari pamoja na Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba
(kushoto kwake), Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
(kulia) na Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda wakati wa
futari aliyoiandaa kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini wa
Manispaa yake, jijini jana.
Mbunge
wa Kinondoni, Iddi Azzan (kulia) akibadilishana mawazo na Meya wa
Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa tatu kushoto) wakati wakipata
futari iliyoandaliwa na Meya huyo kwa wananchi, viongozi wa kiserikali
na kidini wa Manispaa yake, Dar es Salaam jana. Wengine ni Shehe Mkuu wa
Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (wa tatu kulia), Shehe wa Mkoa
wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum (wa pili kulia) na viongozi wengine
wa kidini na kiserikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...