Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuwa wabunifu zaidi na kuhakikisha
kuwa wanachokibuni kiwe kinatekelezwa na kuchukua hatua kwa wasiotekeleza
maelekezo ya kisera pamoja na kuwazawadia wanaotekeleza kwa ufanisi
maelekezo yanayotolewa.
“Watumishi wa Wizara hii tunatakiwa tujiulize tunafanya ubunifu gani ili kuhakisha
wahitimu katika ngazi mbalimbali wanapata maarifa yanayotakiwa na wanaoweza
kusaidia nchi katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali,” alisema Profesa
Mchome.
Profesa Mchome alikuwa akizungumza na Watumishi wa Makao Makuu na Taasisi
zilizoko chini ya Wizara hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre), Ijumaa 18 Julai, 2014
ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi hao na kujadiliana namna
bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara.
Aidha, Profesa Mchome alizungumzia umuhimu wa kuboresha Muundo wa Wizara
hiyo ili kuwezesha namna bora ya kutekeleza majukumu yake baada ya ugatuaji wa
uendeshaji na usimamizi wa shule za Sekondari kwenda kwenye Halmashauri chini
ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na kwa kufuata Hati Idhini iliyounda Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais, Desemba 2010.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akiongea na Watumishi wa wizara yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre), Ijumaa 18 Julai, 2014 ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi hao na kujadiliana namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara.
Mmoja wa Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Grace Naburi akizungumza katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Profesa Sifuni Mchome.
Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Prof. Sifuni Mchome.
Mmoja wa Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Profesa Sifuni Mchome.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...