Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Magese Mulongo (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, jana tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika utakaoanza tarehe 20 hadi 27 Julai Mjini Arusha ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa kongamano hilo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka
Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka alipokwenda kukaguwa Ukumbi wa Ngurudoto, Arusha , jana, patakapofanyika Mkutano wa 45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa kongamano hilo.
Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akitowa maelekezo kwa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika alipotembelea Ukumbi wa Ngurudoto, mkoani Arusha patakapofanyika kongamano hilo ambapo Tanzania ndio mwenyeji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...