SEHEMU YA JENGO LA HOTEL HIYO LIONEKAVYO KWA NJE.
MENEJA WA HOTEL HIYO BI.BEATRICE DALLARIS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI,JUU YA  TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMI KUWA HOTEL HIYO IMEUNGUA MOTO MAPEMA LEO JIJINI ARUSHA.

UTAWALA NA WAFANYAKAZI WA HOTELI YA NAURA SPRINGS YA JIJINI ARUSHA  IMESIKITISHWA KWA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII KUHUSU KUWA HOTELI YETU INAWAKA MOTO NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATU WA MKOA WETU, NDUGU NA JAMAA WA WAFANYAKAZI WA HOTEL ,VIONGIOZI MBALIMBALI, VYOMBO VYA USALAMA, IDARA YA ZIMA MOTO, WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALI MBALII VYA HABARI NA PIA KUSABABISHA WASIWASI NA KUTOWESHA UTULIVU NA AMANI WA MJI WETU.
TUMESIKITISHWA SANA NA TUMEOMBA UONGOZI WA MKOA WETU WALISHUGHULIKIE SWALA HILI KIKAMILIFU KWANI HILI SIO LA KUCHUKULIA MZAHA NA TUNGEOMBA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA HARAKA SANA KWA ALIE TOA TAARIFA HIYO YA UONGO.

TUNAWASHUKURU WATU WOTE WALIOFUATILIA SWALA HILI NAPIA TUNATOA TAMKO KUWA HABARI HIZI ZA KUWA HOTELI YETU INAUNGUA NI ZA UONGO.
BEATRICE DIMITRIS DALLARIS

HOTEL MANAGER

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2014

    Taarifa haisemi hotel ipo wapi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2014

    Huuu ni ushahidi kuwa, baadhi ya taarifa huwa tunazo wekewa kwenye mitandao sio proven kabla hazijawa published.inabidi tujipange upya..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2014

    Pole mpendwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...