Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.
Eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika kama Mabweni ya Wanafunzi wa Shule hiyo,Maabara na Ofisi za Walimu limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kitu chochote kilichoweza kuokolewa.
Jitihada za kuuzima moto huo zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya Waumini wa Kiislam wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za kuuzima moto huo zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya Ultimate,japo baadae gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini hao kulijaza maji gari hilo kwa kurumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto huo ikiendelea.
Chanzo cha Moto huo,inadaiwa ni hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweli la Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.Picha zote na Othman Michuzi.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
Sehemu ya wananchi wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo.
Jitihada zikiendelea.
Gari la Zima Moto mali ya Kampuni ya Ultimate Security likijazwa maji kwa ndoo ili kuendelea na zoezi la uzimaji w amoto huo.
Likafika na gari hili kwa ajili ya kusaidia kuzima moto huo.

Mashuhuda wakiwa nje ya eneo hilo.
Kweli Tanzania, hata magari ya zima moto yanaishiwa maji na kuchotwa kwa ndoo? kwa nini sehemu kama hizo wasijitahidi kuwa na magari sio zaidi ya moja kwa ajili ya matukio kama hayo? hayo ndio mambo ya muhimu sana kujadiliwa hata katika katiba mpya, maana majanga hayo hayabishi hodi wala kutoa taarifa. Wahusika wajitahidi kuona hilo kwa macho mapana. Mungu ibariki Tanzania
ReplyDeleteBongo bad tuko mbali sana na maendeleo. Poleni ndugu wote mliopatwa na janga hili.
ReplyDeleteHow on earth utazima moto na majie ya kwenye ndoo. Poleni wote.
ReplyDeleteInalillahi wainalilaihi rajuun, Allah ataleta wepesi.
ReplyDeletePole sana kwa walimu na wanafunzi pamoja na waumini wa msikiti huo.
ReplyDeleteila kwa nini taasisi zetu km hao zimamoto hazina utayari muda wote kwa ajili ya kukabiliana na majanga!!!
yaani hicho ni kituko cha mwaka huwezi jaza maji kwa ndoo kwenye gari ya zimamoto ili kupambana na moto ulioshika kasi.
Watz tujipange jamani ni aibu kwa Taifa.
Hakika huu ni mtihani tunawapa pole wote waliokutwa na mtihani huu, fasbir sabran jamiiil
ReplyDeleteNini watanzania tumesoma hapa?
ReplyDelete