Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imetenga fedha zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa jamii nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa cha habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”.

“Ni kweli tatizo hilo lipo ndio maana Serikali imetenga fedha tayari ambazo zitagawiwa kwenye vituo vyote nchi nzima” alisema Mwamwaja.

Mwamwaja alisisitiza kuwa deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko Tanga.

Mahabusi hiyo ni miongoni mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii ndani ya Wizara ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 

Matumizi ya fedha hizo ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba wa chakula kituoni hapo ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao na kufikia lengo la kuwarekebisha tabia zao ili wawe raia wema nchini.  

Aidha, Mwamwaja aliongeza kuwa fedha zilizotengwa  si za Mkoa wa Tanga tu bali ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya wazee wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...