Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick
Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa
nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya
kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo
za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati
akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa
nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo
umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu
mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex
Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia
tukio hilo.
Uzinduzi huo ulioandaliwa na
kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji
balimbali wakiwa wameshiriki onesho hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa
muziki huo kwa kiasi kikubwa.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa
nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo
umefanyika
jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu
mbalimbali.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na skwadi lake jukwaani
wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa
uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh
Frederick Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye
na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati
wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la
Shikilia Pindo la Yesu.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria onesho hilo.
Keep up,good job,its a calling,congratulations
ReplyDeleteHongera Rose Muhando kwa kuzindua albamu mpya tunakutakia mafanikio katika kuendeleza kipaji chako cha uimbaji.
ReplyDelete