Basi la kamwana express likilipita lori kwa mwendo kasi karibu na eneo la Chalinze mkoani Pwani huku dereva huyo akijua sheria za bararani kuwa ni marufuku kulipita gari nyingine akijua wazikuwa mbele kunagari inakuja hatua ambayo inasababisha usalama wa abiria na raia kwa ujumla. Picha na Benjamin Sawe Wizara ya Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mkuu Michuzi hapo mmi sioni tatizo kwasababu alama za bara bara zinaruhusu tendo la kuovertake . Hapo kwa sisi waendeshaji magari inasema kea unaweza kulivuka gari la mbele baada ya kuhakikisha usalama uko mbele . Pili alama za bara bara .... mistari miwili white colors mmoja ukiwa na kipande kipande inaruhusu kabisa kuovertake gari la mbele . Hii inamaanisha bara bara hii iko straight haina curve hivyo driver anauwezo wa kuona usalama wake na magari yanayokuja mbele .
    Tatu hii ni sehemu yenye lane mbili upande wa kushoto kabisa ni kwa ajili ya malori yanayoenda kwa mwendo wa taratibu kabisa either wakati wa kupandisha mlima na picha ya kwanza inaonyesha kabisa kuwa driver wa lori amemaliza kipande chake na kinamuelekeza arudi katika lane yake kawaida hivyo driver wa basi alitumia weledi wake kuovertake . Naomba kutoa hoja mheshimiwa Michuzi !
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  2. Annony acha kuongopea watu alama za barabarani katika picha zote mbili haziruhusu kuovertake. hizo white double lines ndio kabisa haziruhusu kuovertake pande zote.
    Hapo chini pia na huwa zinakuwa katika sehemu ambazo dereva hawezi ona mbele vizuri.
    unaweza kuovertake tu sehemu ambazo zina broken/lines, mistari iliyokatikakatika. acha kuongopea watu kabisa, tena ukome.

    ReplyDelete
    Replies
    1. bora umwambie ameandika kwa kujiamini

      Delete
  3. Mdau wa pili umechanganya ............. white line inaruhusu kuhama lane moja kwenda lane nyingine . Umesoma juu juu mstari mmoja ni straight na mwingine ni broken hii inaruhusu kabisa kuovertake baada ya kuona kuna usalama mbele kwanza . Sehemu ambayo hairuhusu kuovertake ni sehemu yenye mstari wa orange hii ndiyo hiruhusu kabisa . Soma vvixuri maelezo yangu naomba kutoa hoja Mheshiwa Michuzi !
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  4. Annony wa kwanza ... udereva umejifunzia wapi au ndio wale mnaonunua leseni bila kujifunza kuendesha gari ...RUDI SHULE

    Annoy wa pili ... asante kwa ufafanuzi mzuri unaoondoa upotoshaji wa huyo jamaa wa kwanza!

    ReplyDelete
  5. annon wa kwanza mtafute mwalimu wako aliyekufundisha maana ya alama hizo, mtandike viboko siku nzima, kama hayupo basi umejifunza mwenyewe, hivyo jiadhibu kwa mwezi mmoja, kwa kuandika hayo hapa umepata faida nyingi, moja kubwa, umejuwa uwezo wako wa kuelewa ulivyo mbaya, na kama wewe ni dereva basi ni dereva unayekaribia kuuwa kwa uzembe hivi karibuni!!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa japan kutokana na picha usemayo sio sahihi: Picha ya juu inaonyesha lori la kushoto likimalizia ile sehemu pana ya kuyapita magari yaendayo speed ndogo mlimani hapo. Hizo yellow lines ukiziangalia utaona ni kama triangle kwani mistari inarudi kukutana na kushoto kabisa kuna arrows white na red zinazoonyesha kuwa left lane inaisha. DOUBLE LANE hairuhusiwi kabisa hata kuigusa moreover kuingia upande wa pili hata kama hakuna gari linakuja mbele. Nafikiri US wanaruhusu kufanya U turn au kuingia/kutoka ktk side roads mijini ila overtaking or driving on wrong side ni kosa kubwa. Kwa picha hiyo ya juu you can clearly see a roli coming. Pia sioni ni wapi kuna msitari mweupe uliokatika hapo.
    Picha ya chini: Makosa ni mawili: kwanza hiyo constant line. Imechakaa na kufutika na sio punctuared. Hivyo uruhusiwi kumpita mtu hapo. Pia, hapo mlima unakwisha so wewe huwezi kujua nani anaweza kutokea mbele. kama wewe ni dereva kweli hiyo lazima uelewe. Kuna nchi hawaruhusi kuovertake au kuweka full light kwenye sehemu za kumalizia milima kama hiyo. Zaidi ya hapo, dereva mzuri hawezi kuovertake wakati haoni picha nzima mbele. Than means red bus anakwenda tu wakati hajui nini kinaendelea kwa blele ya basi la rangi rangi. Iwapo basi la mbele litaona hatari, anaweza kwenda kushoto au kulia na kumwacha Red bus with no time to react. Sorry to say: Nautilia shaka udereva wako. Blackmpingo

    ReplyDelete
  7. MADEREVA WA TANZANIA WANATAKIWA KUPATA MAFUNZO TENA YA NAMNA YA KUENDESHA SALAMA, AU LA SIVYO WATANZANIA WOTE TUTAISHA KWA AJALI.

    ReplyDelete
  8. These lines Does NOT allow you to overtake. Huyo aliye comment hapo juu kweli hajui sheria za barabar.

    ReplyDelete
  9. Hii tabia ya madereva kupita magari inasababisha ajali zisizozalazima katika barabara kubwa. Tujihadhari madereva maisha ya watu ni muhimu.

    ReplyDelete
  10. ANNON NO1 UNAZUNGUMZIA BARABARA IPI HAPO? UDEREVA WA PANDE IPI YA DUNIA UNAOUZUNGUMZIA? MAELEZO YAKO YOTE NI WRONG!

    ReplyDelete
  11. Kabla ya kutoa maoni jipime kama unachotaka kuongea ni sahihi! Nashukuru Mdau wa pili hapo juu kusahihisha, na ndio hao madereva kama hao tunaokutana nao njiani. Ikitokea ajali tunasema kazi ya Muumba!

    Kwa kweli ni balaa juu ya balaa!! Barabara zenyewe ziko chini ya kiwango kuitwa highway (angalia matuta upande wa kushoto picha ya chini), madereva wenyewe mashaka, magari yenyewe siri ya tajiri, na mwisho abiria wenyewe kama kondoo wanaopelekwa machinjioni!!

    Wacha niishie hapo, na sita-comment tena mpaka mwaka kesho! Inachosha!!

    Hivi Michuzi, midahalo ya humu blogini huwezi kutafuta jinsi ya kuifanyia kazi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...