Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Anthony Ishengoma.
Frank Mvungi- Maelezo
Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati za kusafiria za kielektroniki, zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi,  za Maofisa na za kawaida.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara,Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Abdulla Makame  wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Mkutano huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha pia unatarajia kupokea na kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akieleza zaidi Makame amesema mkutano huo utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki,zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi,  za Maofisa na za kawaida za kusafiria.
Aidha Mkutano huo utajadili mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa Dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050.
Pia mkutano huo utajadili mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli mbalimbali zinazolenga kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na kujadili mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.
Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili katika ngazi za kufanya maamuzi ndani ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa Kilele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...