Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa, akizungumza katika hafla waliyowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika kitengo hicho kilichopo ndani ya Jengo la Coco Plaza, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa (katikati), akibadilishana mawazo na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kukutana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenkizinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi na Proctus Ishengoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akifurahi na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi, Mkurugenzi Mtendaji wa muda wa NBC, Pius Tibazarwa na wakili Proctus Ishengoma.
Meneja Mahusiano ya Wateja wa kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha Benki ya NBC, Subira Mwaya (kushoto) akiwa na Wakili wa Kampuni ya Summit Attorneys, Bilal J. Bilal wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla waliowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...