Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria (juu kulia) amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya African paty na mkutano, na sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe.
Pia inasemekana Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki. Taarifa za uhakika za kipolisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt) ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS.
Wakati huo huo taasisi mbalimbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemie za kuwadanganya washabiki na kulivunjia hadhi sifa za bara la Afrika nchini ujerumani ,taasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na m-nigeria huyo Britts Events au Awin Williams Akpomiemie,Pia magazeti mbali mbali ya ujarumani na nchi za kiafrika yameandika BRITTS MAFIA HITS STUTTGART,GERMANY AGAIN !! kusoma mojawapo ya gazeti la Ghana BOFYA HAPA
Polisi wakiwa wamelizingira gari alilokuwemo Diamond na promota wake jijini Stuttgart, Ujerumani, siku ya tukio hilo
Diamond na promota wake wakiondoka eneo la tukio
Mashabiki wakiwa wamezingira gari liliombeba Diamond na promota wake
mnigeria ? kweli wasanii wa bongo mnacheza na maisha,hao wanigeria watawapeleka pabaya
ReplyDeletesasa utapeli kwishney wabongo jichungeni sana
ReplyDeletePole diamond be careful with who you are dealing with in future
ReplyDeleteKWANI WATANZANIA MLIOKO UJERUMANI MNASHINDWA KUANDAA MAMBO KAMA HAYO??
ReplyDeleteWATANZANIA TULIPO UJERUMANI HATUTAKI
ReplyDeletePLAY BACK MUSIC HAPA KISHERIA NI MARUFUKU LIVE TU NDIO INAYORUHUSIWA,WANAOPIGA PLAY BACK WANAIVUNJA SHERIA YA HAKI MILIKI(GEMA)