http://mkumbaru.files.wordpress.com/2012/11/maji.jpg?w=698
Na Julius Konala wa demasho.com,Songea.

WANANCHI wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,wataondokana na tatizo la upatikanaji wa maji lililokuwa likiwakumba kwa muda mrefu hususani kipindi cha kiangazi baada ya kuanza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kitega maji ambao unatekelezwa na kampuni ya Sinani Building Contactors Ltd yenye makao yake makuu mkoani Mtwara katika eneo la Ruhira mjini humo ambapo utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni mbili mpaka kukamilika kwake.

Hayo yalisemwa jana na Meneja ufundi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Souwasa)Manispaa ya Songea Mhandisi John Kapinga,wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari ofisini kwake mjini humo kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa mradi huo.

Kapinga alisema kuwa mradi huo mpaka kukamilika kwake unatarajia kukidhi mahitaji ya wakazi wa Manispaa hiyo kwa asilimia 60,kusukuma maji lita 6500 pamoja na kuhifadhi lita zaidi ya 800,000 za maji jambo ambalo amedai kuwa utasaidia kupunguza tatizo la mgao wa maji kwa wakazi hao.

Alisema kuwa tatizo kubwa linaloukabili mradi huo ni juu ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kumlipa Mhandisi mshauri na Mkandarasi jambo ambalo amedai lisipochukuliwa hatua za haraka linaweza kukwamisha maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ikizingatiwa bado kipindi kifupi cha kuanza msimu wa kifuku.

Nae Mhandisi wa kampuni hiyo ya Sinani Building Contactors Ltd inayojenga mradi huo ,Faustin Otaru alisema kuwa kati ya kazi zinazofanyika hivi sasa ni kuchimba mitalo kwa ajili ya kujenga ukuta katika eneo hilo la mradi lenye ukubwa wa mita za mraba 25,000.

Otaru alizitaja changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wao wa kazi kuwa ni pamoja na kutitia kwa mitambo ya kufanyia kazi,ubovu wa njia za kuingilia magari kwenye eneo la mradi pamoja na ucheleweshwaji wa fedha za kufanyia kazi jambo ambalo amedai kuwa linaweza kukwamisha maendeleo ya mradi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Waandishi wa habari hao katika eneo la mradi baadhi ya wakazi wanaozunguka eneo la mradi huo walisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo la maji na kudai kwamba wameweza kunufaika na kampuni hiyo kwa kupata ajira ambayo imewawezesha kufanya mambo mbalimbali ikwemo kusomesha na kulipa kodi katika nyumba walizopanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huu mradi ukamilike tuondokane na kero za maji ili tuangalie mambo mengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...