

Na Faustine Ruta, Bukoba
Jumla ya wachezaji 26 wa Timu ya Stand United ya Shinyanga wametua mjini Bukoba leo kwa ajili ya kipute cha Ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014-15 na wenyeji wao Kagera Sugar wamefanya mazoezi yao kwa mara ya kwanza Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Wachezaji hao, wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na viongozi wengine, ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi na kesho Jumamosi inataka kuibana Timu ya Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wao ambao pia wanashikilia nafasi ya sita kwenye Ligi hiyo ya Vodacom kwa msimu huu ulioanza hivi karibuni.
Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Kagera wanaingia wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 4 huku Stand United wakiwa nafasi ya 8 nao wakiwa wanalingana pointi na Kagera Sugar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...