Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari (kushoto) akiangalia wananchi wake wakiendelea na uchimbaji wa mtaro wa kupitisha Mabomba ya Maji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kuhakikisha Ahadi ya maji kwa wananchi wa Manyata na Nganana kata ya Usa River inatimia.
Mbunge Nassari aliingia kazini kuanzia asubuhi mpaka jioni. Mradi huu umetoa maji umbali wa kilomita 9 toka kwenye chanzo (Uraki).
Wananchi wa Arumeru walikuwa wanakunywa maji ya majaruba ya mpunga kwa miaka yote kabla ya mradi huo ulioasisiwa na Mbinge wa Jimbo hilo,Mh. Joshua Nassari
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mhe. Joshua Nassari akichota maji katika moja ya bombo mara baada ya kuzindua mradi wa maji aliouanzisha jimboni hapo.
Furaha ya kupata maji ilikuwa ni ya kila mwanakijiji katika eneo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...