Kampuni ya Statoil
Tanzania imewatangaza na kuwazawadia washindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho
katika hafla iliyofanyika siku ya Alhamisi Desemba 4. Mashujaa wa Kesho ni shindano
la biashara lililoandaliwa kwa lengo la kukuza dhana ya ujasiriamali kwa vijana
mkoani Mtwara.
Bwana Nassibu
Hamimu Lilumba ameibuka mshindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho baada ya kutoa
wazo la biashara na kIsha kuandaa mpango wa biashara na kutoa maelezo yake
katika jopo la majaji. Mshindi alizawadiwa fedha taslimu za Kitanzania zenye
thamani ya dola elfu tano (5,000) za Kimarekani katika hafla iliyofanyika
katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mpango wa
biashara uliolenga kufungua kampuni ya utoaji wa huduma za boda boda kwa
utaalamu mkoani Mtwara, uliibuka mshindi kutokana na vigezo ambavyo ni kama
vile fursa katika soko, kiwango cha ushindani wa mwenye wazo, uwezo wa
kusimamia biashara, uelewa wa masuala ya fedha pamoja na fursa za uwekezaji.
Sosthenes
Njelekela, Zawadi Yusuph Washaru, Vivian Charles na Ali Hassan waliingia katika
hatua ya fainali na kupatiwa zawadi zao. Kila mshiriki aliyeingia katika
fainali alijipatia fedha taslimu za Kitanzania zenye thamani ya dola elfu moja
(1,000) za Kimarekani.
Shindano
lilipata muitikio mkubwa kutoka kwa vijana wa Mtwara ambapo vijana 500 wenye
mawazo mbalimbali ya kibiashara katika kilimo, ufugaji wa wanyama na kuku,
teknolojia ya habari na mawasiliano, viwanda vidogo na huduma nyinginezo za
kibiashara walishiriki. Baadhi ya mawazo hayo yalitoka kwa washiriki mmoja
mmoja na mawazo mengine yalitoka kwenye vikundi, kama vigezo vya ushiriki
vilivyoelezea.
Washiriki 40
waliofanikiwa kuvuka mchujo wa awali walipatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambapo
waliweza kujifunza kuhusu njia za kuandaa na kuendesha biashara kwa ufanisi na
namna ya kuandaa mipango ya biashara kutokana na mawazo yao ya biashara.
Mipango hiyo ya biashara ilikusanywa na kupitiwa kabla ya mipango kumi ya
biashara kupelekwa kwa majaji ili kupata mipango mitano ya biashara kuelekea
kwenye fainali. Washiriki wa mipango hiyo mitano walitakiwa kutetea mipango yao
ya biashara mbele ya majaji.
Jopo la majaji
watano liliongozwa na Bi. Victoria Tunu Chale, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
People Dynamics Tanzania LTd na Mhandisi, Bwn. Andrew Mnzava ambaye ni mtaalamu
kutoka Tanzania Renewable Energy Association, Bwn. Mosses Nkanda, Mwanzilishi
na Mkurugenzi Mtendaji wa Mnazi Bay Consulting Ltd ya Mtwara pamoja na Bwn. Justine
Lusasi, Mkufunzi Msaidizi kutoka chuo cha Stella Maris ambaye alishiriki kwa
ukaribu katika kutoa miongozo kwa washiriki wa shindano hilo na pia katika
kusimamia matumizi ya kompyuta zilizotolewa na Statoil kwa ajili ya matumizi ya
washiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho.
“Tuna furaha
kumpata mshindi wa shindano hili. Vijana wengi wa Mtwara walijitokeza kushiriki
katika shindano, jambo lililotupa ari kubwa katika kutekeleza shindano hili. Statoil
ni kampuni inayopenda kuunga mkono vijana wenye vipaji katika nchi ambazo kampuni
hii inafanya shughuli zake. Hii ni njia yetu ya kukuza maendeleo katika jamii
zinazotuzunguka,” alisema meneja wa Statoil nchini, Øystein Michelsen.
Mkurugenzi wa kampuni ya statoil-tanzania bwana Oystein Michelsen iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar uliopo Hyatt Regency Dar es Salaam.Balozi wa Norway nchini Tanzania Mh Hanne Marie Kaarstad akinena jambo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashujaa wa kesho iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar uliopo Hyatt Regency Dar es Salaam.
Bwa. Nassibu H. Lilumba ambaye ndiye Mshindi wa kwanza aliyejishindia dola 5000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...