Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Libundu, Kitongoji cha Nangote,
Kata ya Kiparamnero wilayani Nachingwea katika Kampeni ya nyumba kwa nyumba ya kuwanadi
wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa wilayani humo. Waziri
Chikawe aliwaomba wananchi wa Nachingwea kuwapigia kura viongozi hao
waliopitishwa na CCM kugombea nafasi hizo walizoomba. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika
Desemba 14 mwaka huu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kulia) akimtambulisha kwa wananchi (hawapo pichani), Dastan Likwama
ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nangote katika Kata ya
Kiparamnero waliohudhuria Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika kitongoji
hicho. Waziri Chikawe aliwaomba wananchi hao kumpigia kura kiongozi huyo aliyepitishwa
na CCM kugombea nafasi hiyo. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa
kufanyika Desemba 14 mwaka huu nchini.
Picha
zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...