Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.
Naona Waziri Kivuli Mh Peter Msigwa akiwa wameshikana mikono na Mwana Mfalme Prince Bandar, je Mh. Msigwa alitoa hoja iliyomkosha Mwana wa Mfalme kama kawaida yake?
ReplyDeleteHawa wagombea wanaondelea kufanya kazi za Serikali ni uongo mtupu. Kwingineko wanajiuzulu kwanza. Huo ndio Utawala Bora. Hatuyaoni haya?
ReplyDeleteGood job Nyalandu... You are the best!
ReplyDelete