Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show
wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo
Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo
Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama
vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali
wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii
wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa
mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa
wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu
ijayo Februari 23.
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo
Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...