Katibu mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na
masuala ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen Kayanza akifafanua jambo
wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya Exim jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki, kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo
husherehekewa Machi 8 kila mwaka.
Wakati wa shughuli hiyo wafanyakazi wa
kike wa benki hiyo walitoa wito kwa wanawake nchini kutumia maadhimisho
ya mwaka huu kutokomeza ukatili dhidi ya wafanyakazi wa ndani.
Wanaotizama ni Meneja mwandamizi wa kitengo cha rasilimali watu wa benki
ya Exim, Joan Mbakileki na Mkuu wa matawi wa benki hiyo, Elizabeth
Mayengoh.
Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Elizabeth Mayengoh (kulia), akikabidhi
zawadi kwa Katibu mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali
inayojishughulisha na masuala ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen
Kayanza (wa pili kulia) wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya
Exim jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha siku ya wanawake
duniani ambayo husherehekewa Machi 8.
Wakati wa shughuli hiyo
wafanyakazi wa kike wa benki hiyo walitoa wito kwa wanawake nchini
kutumia siku hiyo kutokomeza ukatili dhidi ya wafanyakazi wa ndani.
Wanaotizama ni Mkuu wa matawi wa benki hiyo, Agnes Kaganda (kushoto) na
Meneja mwandamizi wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim, Joan
Mbakileki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...