Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate, (kulia), na Meneja Miundombinu ya IT wa Mfuko huo, Gilbert W. Chawe, (katikati), wakimsikiliza afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Rehema Kabongo, wakati wa ziara ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mafao ya Uzeeni, nchini Kenya, (RBA), kwenye makao makuu ya PPF barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam.
Maafisa toka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tanzania, (SSRA) na wenzao kutoka Kenya (RBA), wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na mameneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati maafisa hao walipotembelea makao makuu ya PPF kwa nia ya kujifunza shughuli za uhifadhi wa mafao na pensheni.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifuatilia kwa makini wakati wa mkutano baina ya viongozi wa PPF na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao Ya Uzeeni kutoka Kenya, (RBA), walioongozwa na wenyeji wao SSRA kwenye ziara yao ya kujifunza walioifanya makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...