Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya, Dk. Mpoki Ulisubisya akiwaongozwa Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa kuelekea Wodini kumjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya akiwa anamwangalia kwa jicho la huruma Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nacho akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa wakimjulia hali Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Wakuu wa Mikoa ya Mbeya na Rukwa sambamba na viongozi wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya wakiwa wameinamisha nyuso zao huku wakisali kuwaombea watu wenye ulemavu wa ngozi ili wasipate madhara baada ya kumtembelea Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi.
Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake, akiwa anawasikiliza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa waliomfika kuwajulia hali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wanakopatiwa matibabu.
.Waandishi wa habari wakichukua maelezo kutoka kwa wahanga wa tukio la kukatwa kiganja kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino).


Na Mbeya yetu


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya walifika Hospitalini baada ya mtoto huyo kufikishwa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mtoto huyo mkazi katika kijiji cha Ikonda kata ya Chitepa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa alihamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kukatwa kiganja chake akitokea kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani hapa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo, Prisca Shaban(28) alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba usiku alipokuwa anarudi ndani akitokea nje kujisaidia alivamiwa na mtu ambaye hakumfahamu na kisha akamsukumia ndani kabla ya kumpiga kichwani kwa rungu na kisha kupoteza fahamu.

Alisema akiwa amepoteza fahamu mtu aliyekuwa amemvamia ndipo alipata nafasi ya kuingia ndani na kutekeleza adhma yake ya kumkata kiganja mtoto huyo ambaye ni mmoja kati ya watoto watatu wenye ualbino katika familia hiyo na kuondoka nacho.

Alisema wakati hayo yakitokea mumewe aliyemtaja kwa jina la Cosmas Lusambo alikuwa amekwenda kulala nyumbani kwa mke mdogo kwani ilikuwa zamu ya kwenda kulala huko kwa usiku huo lakini baada ya kusikia mayowe ya kuomba msaada alikwenda kuungana na familia yake na kumpeleka mtoto kituo cha afya cha Kamsamba kutokana na kuwa jirani na kijiji chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Akizungumza baada ya kumtembelea Baraka katika wodi ya watoto kwenye hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya, alioneshwa kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.

Alisema ni tukio ambalo linasikitisha ambalo linazidi kuendeleza vitendo vya aibu kwa kuwafanyia ukatili wa kinyama albino kwa ujinga wa watu wachache wanaowadanganya watu kuwa viungo vyao ni bahati ya kuleta utajiri.

Mhandisi Manyanya mbali na kuzungumza na familia ya waathirika wa janga hilo pia aliongoza sara fupi ya kuwaombea albino hospitalini hapo alionesha pia kusikitishwa na mwenendo wa mashitaka ya watu waliofanya ukatili dhidi ya albino akisema mahakama zimekuwa na milolongo mirefu inayokatisha tama wadau wa kupinga ukatili huo.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri pia kuangaliwa upya kwa sheria inayohusu masuala ya hukumu za kifo akisema ikibidi inapaswa kubadilishwa ili iweze kutoa haki kwa watu wanaofanya ukatili dhidi ya wenzao.

Alisema sheria ya sasa kumtaka rais pekee kuwa mtu wa mwisho kutoa uamuzi kunyongwa kwa mtu aliyehukumiwa inakosa nguvu ya kutekelezwa kutokana na majukumu mengi aliyonayo na kushauri kuwa ni vyema vyombo vya sheria vipewe mamlaka ya mwisho ya kutekeleza adhabu hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tuna makachero wengi hapo Tz, wawatumie wale makachero wanaobugudhi viongozi wa siasa kutafuta hawa wanaodhulumu nafsi za walemavu wa ngozi.

    ReplyDelete
  2. Why is this allowed to happen, it is a disgrace. The Government should do something urgently!! Please!!

    I cannot comprehend how this could happen in this century with all the government machinery around, what are the police doing?

    ReplyDelete
  3. Pole sana mtoto, pole pia kwa wazazi.
    Sifikiri kama nimewahi kuona hivi karibuni jambo ambalo limenitia majonzi kama tukio hili.Kwa umri wangu na kazi nilizofanya nimeona mengi ya kutisha, lakini this is the worst. Think of the fear and desperation that the little man had when they grabbed him and possibly put his hand on a kigogo na kumkata mkono kwa panga. Audhubillah.Wabongo wote we are guilty here. Naomba waziri mkuu alipe fidia kwa kijana huyu kwa niaba yetu.

    ReplyDelete
  4. Only death sentence is appropriate for these crimes.

    ReplyDelete
  5. Death sentence? Oh no, dont do them a favour.I was thinking of something more appropriate, say Mathew 5:38.
    ibrahim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...