Uongozi wa shule ya sekondari ya Kutukutu iliyopo wilayani kilosa
mkoani Morogoro, umeishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa
msaada wa vitabu vya masomo ya sayani.
Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni mbili umekabidhiwa hivi
karibu na wawakilishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikiwa ni
mpango wa SHULE YETU unaosimamiwa na kampuni hiyo.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo
mkuu wa shule ya sekondari Kutukutu Finyilise Elias amesema, utasaida
kuongeza ufaulu wa wanafunzi wake wanaosomea masomo ya sayansi.
Mwalimu Finyilise amesema, kumekuwa na ufaulu wa kusuasua kwa
wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne hasa kwenye masomo ya sayansi
hivyo msaada huo utasaidia kuongeza ufaulu shuleni hapo.
“ Wanafunzi wetu wanaosomea michepuo ya sayansi wamekuwa na ufaulu
mdogo sana na hii inatokana na ukosefu wa vitabu vya masomo hayo kwa
muda mrefu sasa” alisema Mwalimu Mkuu huyo.
“msaada huu utatusukuma haraka kwenye ufaulu wa kiwango cha juu wa
masomo ya sayansi kwani mwitikio wa wanafunzi wetu ni mkubwa na
tunatarajia tutapata matokeo ya haraka kutokana na msaada huu wa
vitabu” aloingeza Mwalimu Finyilise.
Awali akikabidhi msaada wa vitabu hivyo, Meneja wa Airtel Mkoani
Morogoro Bw. Omar Bongo amesema, hatua hiyo ni kuwawezesha wanafunzi
wa shule za sekondari kupata maarifa ya masomo ya sayansi kwa vitendo.
“Sisi wa Airtel tumekuja hapa kusukuma gurudumu la maendeleo mbele
kupitia elimu na hasa vitabu vya kujifunzia, mkazo wetu kwa sasa ni
masomo ya Sayansi na tumeleta vitabu vya kujifunzia. Alisema Bw.
Bongo.
Shule hiyo ya sekondari kutukutu yenye wanafunzi zaidi ya 300 bado
inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na vyumba vya maabara
na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Wanafunzi wa shule ya sekondari
Handeni iliyopo wilayani Handeni wakisoma vitabu vilivyotolewa na
Kampuni ya Airtel shuleni hapo kwa ajili ya masomo ya sayansi vyenye
thamani ya sh.milioni mbili.
Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Airtel Kanda,Aluta Kweka kulia akimkabidhi Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweymamu vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kampuni hiyo vyenye thamani ya sh.milioni mbili anayeshuhudia katikati ni Mwalikishi wa Afisa Elimu wilaya ya Handeni,Ally Mwinyuma ambaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Handeni,Ally Adamu kulia akimkabidhi kitabu mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Aisha Juma cha Fizikia ambavyo vilitolewa na kampuni ya simu za mikononi nchini Airtel vyenye thamani ya sh.milioni mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...