Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni Rasmi
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda ameitaka mifuko ya jamii kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi kujiunga na mifuko hiyo ili kuweka akiba ambayo itasawasaidia kwa maisha yao ya baadaye.
Aliyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika mjini hapa uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo
.
Alisema kuwa, mifuko hiyo ina manufaa makubwa sana kwa jamii hususan kipindi cha kustaafu ambacho huwa ni kipindi kigumu sana kwa asilimia kubwa ya wastaafu ambapo wengi wao mifuko hiyo huwasaidia sana kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.
Ntibenda alisema kuwa, kuna idadi kubwa sana ya wastaafu ambao wangependa kujiunga na mifuko hiyo ila kinachowawia ugumu ni kutopata elimu ya kutosha juu ya kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana kwao.
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina alisema kuwa ,mfuko huo umeanza kutoa elimu nchi nzima juu ya mabadiliko ya mfuko huo ambapo wamezindua mafao mapya manne ambayo ni fao la elimu,uzazi,fao la kuanza maisha ,na fao la kujikimu ambapo mafao hayo yote ni yataanza kutumika katika mfuko huo hivi sasa.
Aloyce amesema kuwa,mfuko huo wamekuwa wakijitahidi sana na kukabiliana na changamoto ya wajiri kutofikisha mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa wakati ambapo mfuko huo wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha makato hayo yanafika kwa wakati na muda ulipangwa .
Aidha washiriki wa mkutano huo, wakizungumza kwa nyakati tofauti waliutaka usimamizi wa mifuko hiyo kuongeza mifuko zaidi ili wananchi wawe katika hali nzuri ya kiuchumi kwa kutumia mifuko mbalimbali na kuondokana na kusongamana kwenye mifuko michache iliyopo .
Meneja wa mfuko huo kanda ya kaskazini ,Denis Kaitwa amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kutoa elimu kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kuwa wagumu kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwa maisha yao.
Kaitwa alisema kuwa,kupitia mkutano huo utawawezesha wadau hao kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi wao na hatimaye kuweza kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wa GEPF ambao una manufaa makubwa kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...