Mtafiti wa
Lugha za alama Profesa Henry Muzare akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo katika ukumbi wa habari MAELEZO,kuhusiana na umuhimu wa lugha
za alama kwa viziwi na jamii,(kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi
Tanzania (CHAVITA)Dicksom Mveyange.
Mkalimani wa Lugha za alama Octaviani Simba
akimtafsiria lugha za alama Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA),Dicksom Mveyange,leo katika
ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)
(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)
Na Avila
Kakingo,Globu ya Jamii.
CHAMA cha viziwi
Tanzania(CHAVITA),waomba ushirikiano kwa jamii kuwasaidia watu wenye uziwi kwa
kuwa wengi huwatenga kutokana na kutoelewa vitu vinavyoendelea.
Hayo
yamesemwa na Mtafiti wa Lugha za alama profesa
Henry Muzare wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa
Lugha za alama kwa viziwi na jamii zima leo katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Muzare
alisema luwa binadamu anahaki ya kutumia lugha anayoimudu ili kuwasiliana na
watu wenginekatika jamii, lugha hizo ni pamoja na alama wanazozitumia viziwi.
Vitendo
vyovyote vinavyomnyima mtu fursa ya
kutumia lugha anayoimudu vizuri inatafsiriwa ni kumnyanyasa alisema Muzare.
Muzare amesema
kuwa katika mfumo wa elimu ya mjumuisho
unaotumika kwa kuwachanganya viziwi na
wanaosikia bila kuwa na msaada au huduma yeyote hali hiyo inawafanya watu wenye
uziwi kuishi maisha ya kubahatisha, pia
hali hiyo inakatisha tamaa kwa watu hao wakiwa shuleni na chuoni, kwa kuwa
walio wengi hawaelewi mambo yanayofundishwa.
Aliongezea
kuwa kwenye huduma za kijamii kama hospitali, mahotelini, sokoni hata kwenye
vyombo vya mawasiliano mfano luninga,watu wenye uziwi wanahitaji mkalimani ili kupunguza hali
ya watu hao kukosa haki zao za lugha yao wanayoielewa kwa ufasaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...