Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama tarehe 21 April 2015 alifanya Ziara ya
Kiserikali katika Bunge la Zambia. Dhumuni ya ziara hiyo ilikuwa ni kujifunza taratibu na mambo mbali mbali yanayohusiana na Bunge la
Zambia. Katika ziara hiyo Mhe Waziri aliongozana na Balozi wa
Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi Grace J. Mujuma.
Mhe. Jenista Mhagama na Mhe Balozi Grace Mujuma wakipewa
maelezo na Spika wa Bunge la Zambia Jaji, Dkt. Patrick Matibini
(hayupo pichani).
Mhe. Jenista Mhagama alipata nafasi ya kuutembelea Ubalozi wa Tanzania Lusaka na kusaini kitabu cha wageni. Mhe Balozi Grace J. Mujuma wakifurahi jambo na Mhe Waziri Jenista Mhagama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...