Home
Unlabelled
YALE YALEEEE........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hawa madereva inavyoelekea hawajui maana ya hiyo mistari miwilli ya katikati ya hiyo barabara, katika hizo picha mbili za mwanzo kama wanafahamu maana yake nini na wanafanya makusudi basi wanastahili adhabu kali,itakayowakumbusha madereva wengine wasiotii sharia za barabarani.
ReplyDeleteOna ona kuna kupona hapo tena hii ni makusudi kabisa
ReplyDeleteKamanda mpinga ushahidi wakutosha upo kwenye picha. Aanza na hawa na hamasisha jamii waedelea kutuuma picha kama hizi ili ufanya kazi yako
ReplyDeletePicha hizi na hata matukio yote yanayotokea hakuna anayejali kwa kuwa wenye mabasi hawajahusishwa. Dawa ya hawa madereva wazembe ni kuifungia/ kuinyang'anya leseni ya kampuni husika, hapo ndio utaona wenye mabasi wataacha kuajiri watu wasio madereva. Nakumbuka Waziri wa Uchukuzi aliyepita atoa kusudio kali kwa mmliki wa basi lilosababisha ajali mbaya sasa Tabora. Sasa ni vema wadau tukafahamu kuwa madereva wote wazembe, hayo mabasi wanayoendesha sio yao, wamekadhiwa na wamiliki. Wamiliki wote wenye mabasi yanayosababisha ajali za kizembe, utakuta wamewapa hawa madeiwaka kwa sababu hawahitaji malipo mazuri. Wanalipwa chochote kwa kuwa nao wanajifunzia kuendesha kwenye roho za watu. Ni vizuri Serikali ifikie wakati wa kuwajisha wamiliki ili kukomesha ajali. Inatakiwa kampuni yoyote itakayosababisha ajali ifungiwe angalau miezi sita mpaka mwaka mmoja, kama wanavyofanya wenzetu nchi zilizo endelea. Pia inatakiwa ufanyike uchunguzi wa kutosha ili kampuni isibadilishe jina.
ReplyDeleteHawa wenye mabasi hawana huruma kabisa na roho za wabongo, wangekuwa na huruma wangewalipia mafunzo madereva wao wiki iliyopita wakati Serikali ilipoamuru kila dereva arudi shule. Nakumbuka ni kampuni moja ile iliyosababisha ajali Iringa ndio iliwapeleka madereva wake shule.
Tunaiomba Serikali itazame upya wa kuwalazimisha hawa madereva kurudi shule. Ziko njia nyingi sana za kufanya hivyo, mojawapo ni kutoa agizo kwa wamiliki wa mabasi, kuwapa muda maalum ya kuwa madereva wake wote wawe wamerudi shule. Serikali inaweza kusema katika kipindi cha miezi sita, kufika mwezi wa kumi haitaruhusu basi lolote kuendeshwa na dereva asiye na cheti cha Chuo cha Usafirishaji.
Waheshimiwa Wabunge kwa kuwa wao wana mashangingi na hawatumii haya mabasi, ndio maana hawaoni hata haja ya kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuepusha janga hili la Taifa, wako tayari kupeleka hoja binafsi ya vijana kuliko mzimu huu unaomaliza wananchi kila siku. Hebu wabunge fikirini, mnapoteza wapiga wangapi kila siku kutokana na janga hili.
Project hiyo ya shetani. Amekamata akili za watu
ReplyDeletewameambiwa waende kusoma wanagona. Wanaelekea alama za barabarani hawazijui. Hii ni janga kabisa.
ReplyDeleteNingekuwa mwajiri. hao hawana kazi
ReplyDeleteWamekataa kwenda shule wakati hawajui hata alama za barabarani. Hivi, picha haziwezi kutumiwa kama ushahidi ili watu waadhibiwe?
ReplyDeleteTena ni dereva wa Shirika la Umma SU 37306 huyu anatakiwa afukuzwe kazi na kutolewa mfano.
ReplyDeleteHAWANA UJUZI WA MATUMIZI YA BARABARA WAO BORA LIENDE TU NDIO MAANA AJARI ZIMEKUA NYINGI, MIE INANIUZI SANA HII MIDEREVA FEKI
ReplyDeletehili jamabo kwa sasa halina suluhisho , na kuna mengi yanakuja kama vile majengo kuanguka, barabara kubomoka kabla ya muda, watu kufa hospitali kwa makosa ya kimatibabu, watu kufa kwa kula chakula kichafu/kutumia bidhaa mbovu.
ReplyDeleteNi tatizo la kimfumo ambalo limekuwa likijengwa na sasa matokeo yake ndo tunayona, kurekebisha tatizo hili inahitaji miaka mingi kama ili iliyotumika kuharibu mfumo mzuri tuliokuwa nao na kutufikisha hapa.kwa mfano kurekebisha mfumo wa elimu inahitaji miaka kama 25 hivi kuanzia sasa ili tupate mfumo unaonfaa na kutoa mazao mazuri yatakayoleta maendeleo ya nchi. inabidi tufikirie namna ya kufanya MAPINDUZI na baada ya kupata hiyo namna tuyatekeleze hayo mapinduzi ndio tutafanikiwa