Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 
Mhe. Kavakure aliwasili nchini tarehe 03 Mei 2015. Wakati huo huo, Mhe. Membe ataongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda Burundi siku ya Jumatano tarehe 06 Mei 2015 kufanya mazungumzo na Serikali ya Burundi kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na 
Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam 
04 Mei 2015

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.


Ujumbe wa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia mazungumzo hayo kabla ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Membe kwa heshima ya


mgeni wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2015

    Majirani wawasaidie watu wa Burundi wasije wakarudi nyuma. Huu siyo wakati wa nchi yoyote tya kiafrika kuingia katika vurugu bali ni wakati wa kuleta maendeleo. Uchaguzi ni tukio lipite kwa amani bila kuvuruga maisha ya wananchi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2015

    Afrika mashariki iwe uwanja wa amani na maendeleo siyo nchi zenye vurugu hazisaidii maendeleo ya wenyenchi hata kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...