Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza na
wanamichezo kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika
Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo
na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black
Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Nachingwea, Mhe Pololeti Mgema.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji
wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo
kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa
Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka
kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1.
Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni wa Timu ya
Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja
na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema,
baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya
Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini
Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria
fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo
kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na
wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na
wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto
aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...