Kampuni ya Hifadhi Builders iliyokuwa na mradi mkubwa nchini inayoitwa Dege Eco Village wameweza kushiriki vyema maonyesho ya maonesho 39 ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Dege Eco - Village, Bi. Catherine Mhina alisema kwamba Dege Eco Village wanafurahi sana kuweza kuwafikia watanzania wengi ambao walikuwa na shauku ya kujua huduma wanazo zitoa iki ni pamoja na kununua nyumba wanazojenga katika mradi wao.
"Tunashukuru Kila mmoja alikuwa akipita hapa anapenda kujua huduma zetu na pindi unapompa maelezo ya kina hasiti kujaza fomu ili aweze kununua nyumba."
Aliongezea na kusema kwamba mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Ras Dege, Kigamboni itakuwa na huduma za kijamii kama hospitali, shule aina ya chekechea, sekondari, pia kutakuwa supermarket na kadhalika.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village akimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village wakiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...