Daktari Bingwa wa Watoto na magonjwa ya figo, Jacquline Shoo akitoa
maelezo kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika
kikao cha kuhitimisha (Exit Meeting) la huduma za madaktari Bingwa hapa nchini.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akishuukuru
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili katika kikao cha kuhitimisha zoezi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey, akizungumza na timu ya madaktari Bingwa na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, kikao cha kuhitimisha zoezi hilo.
Zoezi la huduma za madaktari bingwa liliodhaminiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili limehitimishwa mwishoni mwa wiki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katika zoezi hilo la siku tano jumla ya wagonjwa 740 wamepata huduma na wagonjwa 24 wamefanyiwa upasuaji.
Akizungumza katika mkutano wa madaktari na timu ya uendeshaji ya hospitali hiyo kabla ya kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey amewashukuru madaktari Bingwa kwa uzalendo wao na kuitolea kufanya kazi katika mazingira magumu.
Aidha amewahimiza madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kuhakikisha kuwa dawa zote muhimu zinapatikana wakati wote.
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Mfaume Salamu, kwa niaba ya uongozi wa Hospitali hiyo ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika hospitali hiyo na kuwapa uzoefu madaktari wake. Amesema ujuzi waliopata katika kipindi hicho cha siku tano utawasidia kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa watakaokuja kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Zoezi hilo sasa linahamia katika mkoa wa Simiyu kuanzia tarehe 06 hadi 10 Julai, mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...