KOCHA Mfaransa, Patrick Liewig, akizungumzia mikakati yake ya kiufundi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu ya soka ya Stand United ya Shinyanga, kwenye makao makuu ya kampuni ya Acacia jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 20, 2015. Mkataba huo ni chini ya udhamini mnono wa kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi mitatu ya kuchimba dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara
Na K-VIS MEDIA
KLABU
ya soka ya Stand United ya mjini Shinyanga, imesaini mkataba wa miaka miwili na
kocha Mfaransa, Patrick Liewig, ili kuinoa timu hiyo itakayoshiriki ligi kuu
soka Tanzania bara msimu huu.
Akizungumza
wakati wa kutiliana saini mkataba huo kwenye ofisi za wadhamini wakuu wa timu
hiyo, Acacia, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2015, mwenyekiti wa Stand
United, Amani Vincent alisema, baada ya kuangalia vigezo mbalimbali ambavyo klabu hiyo ilihitaji, imeridhika pasina shaka kumuajiri kocha huyo, ili ainoe timu yake kwa misimu miwili.
“Kocha
huyu kama mjuavyo anayo sifa ya kuinua vipaji, na sisi tunataka kutengeneza
vipaji kutoka chini ili wachezaji hao waweze kuichezea timu yetu”, amesema.
Kocha
huyo aliwahi kuifundisha Simba ya Dar es Salaam, kwa miezi sita kabla ya
mkataba wake kusitishwa.
Stand
United ambayo inashiriki ligi nkuu ya soka Tanzania bara kwa mara ya pili, hivi karibuni ilipata udhamini mnono kutoka kampuni ya uchimbaji madini, Acacia.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Liewig, amesema, atahakikisha anajenga msingi mzuri timu
hiyo kwa kuwa na timu ya kikosi cha wachezaji chipukizi ili iwe na hazina ya
wachezaji. “Kinachohitajika ni kuwa na subira, kwani ninataka kujenga timu na
kazi hii siyo ya mara moja.”amesema.
Pamoja na mabo mengine, udhamini wa Acacia kwa timu hiyo ni pamoja na malipo ya kocha.
MWENYEKITI wa Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent, (wapili kulia), akibadilishana hati za mkataba na Kocha Mfaransa, Patrick Liewig, makao makuu ya kampuni ya Acacia, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 20, 2015. Kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Acacia, Frederick Njoka
Liewig, (kushoto), na Amani Vincent, "wakimwaga" wino
Mwenyekiti wa Stand United, Amani Vincent, (kulia), akizungumzia maudhui ya mkataba huo na uamuzi wa klabu yake kumpatia "kandarasi"kocha huyo
Liewig, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
Frederick Njoka, akifungua mkutano huo wa waandishi wa habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...