MWANASIASA mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Julai 8, 2015, Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’, alionya
Amesema, CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.
“kuna kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema Mzee Kingunge.
"CCM lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye uchaguzi".
Hivi karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.
Hata hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao vya chini.
One cannot take sides in a contest and yet gain respect as a neutral adviser to that contest or its contestants. It's simply not possible.
ReplyDeleteKomrade na babu yangu niliyekuwa nakutazama kama Mwalimu Nyerere linapokuja suala la wakulima na wafanyakazi watu wanyonge ambao ni ndiyo wengi Tanzania upo busy na watu wa tabia zinazotia wasiwasi, watu uliowapinga wakati ule. Wewe ni sio Paulo kwenye njia ya Damascus bali Mugo wa Kibiro kwenye Riwaya ya Ngugi wa Thiong'o, The Grain of Wheat.
ReplyDeletemzee wetu hapo umechemka...wewe ni team Lowassa umeshaliweka wazi. Umepoteza nafasi yako as a wise man, umeshawekwa mfukoni
ReplyDeleteTusubiri tusikie mengi mwaka huu. Ni kazi kweli kweli. Mzee mstaafu na kijana aliye kwenye ngazi za juu za uongozi wa chama wananyukana. Mmmh. Sijui itakuwaje?
ReplyDeleteYou said it all Anonymous
ReplyDeleteWafanyiwe debate kama weanvyo fanya wama rekani. Waanike sera zao na wananchi / wanachama wa CCM waamue yupi anafaa.
ReplyDeleteMzee wetu naona huko unakoenda sasa ni uzee hasi kwani siyo wewe tuliyekujua wakati tunakua. yaani umefikia hatua unaunga mkono watu wenye madoa ya rushwa yaliyokomaaa. kweli baba Wa Taifa (Mwalimu Nyerere) akiamka leo hii na kusikia uliyosema na msimamo uliyoutoa siku chache zilizopita za kuunga mkono Fisadi, duh atahama CCM kwa ajili yako.....
ReplyDeleteY=a+bx+e
ReplyDeletewhereby Y = moral authority
a = integrity
b = credibility
x = variable which can take any value (either 1=clean, 0 = corrupted or under influence)
e = white noise (error term after all we are all human)
Listening to Mzee Kingunge with recent political developments, I failed to understand.him. the equation above doesn't balance.
The error term is so huge that it can't be ignored as insignificant.
Wenye uwezo wa kuongoza wako wengi katika hao 38 waliobaki.
ReplyDelete