Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services, jana imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya ada kwenye shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao inayoendeshwa na taasisi hiyo.
Wanafunzi hao ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na Joceline Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama yao aliyejulikana kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha miaka mitatu mfululizo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura,akionyesha moja fomu maalumu zinazotumiwa na wateja wao katika hautua za awali wakati wa uombaji wa mkopo kupitia taasisi hiyo. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...