Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama), akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani, Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao.
 Sehemu ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.
 Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5, mwaka huu mjini Singida.
Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mkoani Singida walioshiriki katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao. Wa tatu kutoka kulia (Waliokaa kwenye viti) ni Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati – Singida na Kulia kwake ni Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani. Semina ilifanyika Septemba 5, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...