Wafanyabiashara
wamehimizwa kutumia mtandao wa internet kutangaza bidhaa na huduma
wanazotoa kwa kuwa njia hiyo ni nafuu na inawafikiwa watu wengi kwa
haraka. Hayo yalibainishwa na Bw. Dickson Inachee, Raia wa Uganda
alipokuwa anatoa mada katika kongamano la siku mbili la Watanzania
wanaoishi Uingereza lililomalizika jijini Birmingham siku ya Jumamosi
tarehe 05 Septemba 2015.
Bw.
Inachee alieleza kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya watu
milioni 9.3 wanatumia internet nchini Tanzania. Kati ya hao watu milioni
2.4 wanatumia mtandao wa face book, hivyo ukitangaza katika face book,
tangazo lako litawafakia watu wengi kuliko kutumia vyombo vilivyozoeleka
kama magazeti.
Aliendelea
kueleza kuwa tangazo katika face book linatozwa Dola moja ya Marekani
na kwa Tanzania litawafikia watu milioni 2.4 lakini tangazo hilo hilo
ukilitoa katika gazeti linalopendwa sana nchini Tanzania utatakiwa
kulipa Dola 300 na litawafikia watu elfu 50 tu.
Bw.
Inachee alimalizia mada yake kwa kusisitiza kuwa, endapo wajasiliamali
nchini Tanzania wanataka kufanya biashara kwa kutumia mbinu mpya za
kibiashara, basi hawana budi kutumia internet kutangaza bidhaa zao kwa
kuwa njia hiyo itawaondolea mzigo wa kulipa fedha nyingi katika vyombo
vilivyozoeleka sanjari na kuwafikia watu wengi zaidi.
![]() |
Bw. Anthony Chaula akiwasilisha mada
Katika
hatua nyingine, wanadiaspora walioshiriki kongamano hilo, wameridhishwa
na hatua ya Serikali ya kuwapa hadhi maalumu katika Katiba
inayopendekezwa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...