Na: Hassan Hamad, OMKR.

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar kukutana, ili kutatua mzozo wa kisiasa uliojitokeza.

Amesema Zanzibar ni nchi amani, hivyo hakuna haja ya kuruhusu migogoro ya aina hiyo ambayo inaweza kupelekea kuvurugika kwa amani na kuipotezea sifa Zanzibar katika jamii ya Kimataifa.

Jaji Mutungi akiambatana na baadhi ya wajumbe wa ofisi hiyo ya msajili pamoja na msajili wa vyama kwa upande wa Zanzibar Bw. Rajab Baraka, ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Amesema kuna kila sababu ya kulinusuru taifa kuingia katika migogoro isiyokuwa ya lazima, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kumaliza tatizo hilo.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, amesema amekuwa akichukua juhudi binafsi kukutana na wagombea wenzake kuzungumzia tatizo hilo, lakini baadhi yao wanaonekana kutokuwa tayari kulizungumza.

Amesema hapendi kuona Zanzibar inaingia katika machafuko yanayoweza kuepukwa, na kwamba viongozi wengine pia wanapaswa kufikiria amani na maslahi ya Zanzibar kuliko maslahi binafsi.

Katika hatua nyengine Maalim Seif amemshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bw. Jecha Salim Jecha kwa kuiingiza nchi katika migogoro ya kisiasa na kikatiba.

Akinukuu vipengele vya Katiba ya Zanzibar, Maalim Seif amesema kipindi cha Urais wa Zanzibar ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kuapishwa, hivyo kuanzia tarehe 02/11/2015 kipindi cha Urais wa Zanzibar awamu ya saba kitakuwa kimemalizika. 

Hivyo amesema bila ya kuchukuliwa juhudi za dharura, kuanzia tarehe 02 mwezi ujao kwa mujibu wa katiba, Zanzibar itakuwa haina Rais, Serikali wala Baraza la Wawakilishi.
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa Ofisi hiyo. Kushoto ni msajili wa vyama Zanzibar Bw. Rajab Baraka. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mzee mnafikiri huyu kashalikologa sasa anajifanya kutafuta suluhishi hivi watanzania tunasahau haraka ni juzi huyu mtu kufanya kosa la kujitangazis matokeo kinyume na taratibu za uchaguzi anataka kutuambia hazijui na yeye yumo kwenye serikali iliyoziweka taratibu hizo kwanza achukuliwe hatua za kisheria

    ReplyDelete
  2. Penye wazee haliharibiki neno, visiwani mjipange kumaliza mchakato kwa amani.

    ReplyDelete
  3. Cha kushangaza Marais wote waili wako kimya hawajasema kitu japo warais wa demokrasia duniani wandhani uamuzi utenguliwe.

    ReplyDelete
  4. Wachunguze uhalali wa kura zake,kama sio za ujanjax2 kutoka kwenye kitengo cha Ukawa IT, then waangalie adhabu ya mzee kuvunja sheria ya uchaguzi kwa kujitangazia ushindi mbele ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa.
    Akivuka hayo yote mpeni ushindi wake.

    ReplyDelete
  5. Hiki ni kitahanani cha peke yake, binafsi nazidi kumuomba Mwenyeez Mungu atujaaliye salama na amani katika hili na kulivusha salama wa salimini jambo hili ili ndugu zangu wote wa visiwan (Unguja na Pemba) washuwarike roho na nafsi zao, kuliko hiki kizaazaa cha mtu mmoja kuleteleza yote haya. Laitani ingekuwa hata thawabu zinapatikana kwa kung'ang'ania madaraka au kuyataka kwa nguvu, basi tungesema wengine ni wa peponi moja kwa moja, lakini abadan! Badala yake tunasahau kuwa yote haya ni ya kupita na pia ni mtihani mtupu katika dunia hii, khususan pale tunapo yapata au kuyatumia kinyume na uhalali wake wa tunavyoyapata ama kuyatumia. Binaadam hapa tulipo hatulijuwi la sasa hivi, baadae wala khalafu, la kesho wala lijalo, kwa nini basi tusikubali kushida ama kushindwa na maisha yakaendelea kama kawaida na kuwa na wamani na utulivu kwa raia wote nchini, maana tutambuwe hili sio la visiwani peke yao, linatuweka roho juu takriban nchi nzima (Bara na Visiwani). In Sha Allah, Mwenyeez Mungu siku zote hamfichi mnafiki humdhihirisha kwa namna ama njia yeyote ile kwani yeye ndiye mwenye kuziona nafsi zetu, mwenyekujuwa ya ghaibu na bayana. So I believe HE knows what and where went wrong na kwa kudra zake juu ya hili atatujaaliya wepesi na kulivusha kwa salama.

    ReplyDelete
  6. Kusema kashinda alikuwa hajitangazii ushindi bali alikuwa akitekeleza uhuru wake wa kauli kujieleza mawazo yake.

    Na alisema tume itangaze, hakusema anatangaza.

    Hakushinikiza tume, alisema anaomba. Hakuipa tume sharti lolote.

    Bali tunaona kuna watu wameishinikiza tume isitangaze matokeo na ivuruge uchaguzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...