Logo ya Zadia
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu. Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.

Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.

Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.

ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.

Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.

ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.

Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki, Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ni vyema kwa amani ya Zanzibar; tuache sheria za nchi zifanye kazi yake. Taasisi zinazojidai kuwakilisha jamii ziache kushika mlengo au mashinikizo kutoka kwa mtu au chama fulani. Zanibar ni yetu sote ; Tanzania ni yetu sote.

    ReplyDelete
  2. Taasisi zisitumike kwa malengo ya mtu binafsi; sheria za nchi na katiba ndio cha kusisitiza kifatwe. Hakuna mwenye Uzanzibari zaidi ya mwengine.

    ReplyDelete
  3. Ni vyema kwa amani ya Zanzibar; tuache sheria za nchi zifanye kazi yake. Taasisi zinazojidai kuwakilisha jamii ziache kushika mlengo au mashinikizo kutoka kwa mtu au chama fulani. Zanibar ni yetu sote ; Tanzania ni yetu sote.

    ReplyDelete
  4. Miye nashangazwa sana na jamaa wanaosema wao wakipenda sana kibanda chao cha makuti lakini waishi kwenye ghorofa ya kupanga.

    ReplyDelete
  5. INAELEWEKA KUWA HAO WANAOJIITA ZADIA NDIO WALE WALE WAPINZANI WA SMZ WALIOKIMBILIA NJE YA NCHI.
    SASA NINAWAULIZA , JE NI HAKI WIZI AU ONGEZEKO LA KURA KUFANYIKA KATIKA UCHAGUZI, YAANI KURA ZILIZOPIGWA KUWA NYINGI KULIKO IDADI YA WALIOANDIKISHWA KUPIGA KURA? KAMA NI HIVYO BASI MAALIM APWE.
    LAKINI SISI VIZAZI VYA WANAMAPINDUZI HALISI TUNASEMA KATU NCHI HII HAITOINGIA MIKONONI MWA WALOWEZI KWA NJIA ZA GHILIBA.

    ReplyDelete
  6. Thanks be to ZADIA for your good advice particularly to our President of Tz on using his authority to preserve peace and harmony in Zanzibar and Tz in general. I love my countr.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...