Mtu mmoja amenusurika kifo kufuatia ajali ya gari alilokuwa anaendesha mchana huu kwenye milango ya saa 8.10. katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva huyo ambaye alishindwa kuidhibiti gari ndogo aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili Z 511 FG na gari kuacha barabara na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto.
Dereva huyo, ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake.
Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu. (kutokana na maadili ya taaluma ya habari sikuwaletea picha ya dereva ambaye alikuwa peke yake ndani ya gari hiyo ila gari ni kama inavyoonekana kwenye hizo picha. Picjha na mdau Hassan S.
Sehemu ya nyuma
Sehemu ya ubavuni
Sehemu ya mbele
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...