Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atafanya ziara katika Hospitali ya
Taifa Mhimbili Kesho Jumatatu (23 Novemba, 2015) kuanzia majira ya saa nne
asubuhi.
Ziara hiyo ni kwa
ajili ya kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyeagiza fedha zilizochangwa ajili ya hafla
ya wabunge zitumike kununulia vitanda vya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasilino,
IKULU
20 Novemba, 2015
Sawa mkuu tuko nawe. Hii safi sana. Mungu awatie nguvu na kuwalinda.
ReplyDeleteWazo zuri sana naipongeza serikali.kwa hlo
ReplyDeletehizi press releases zingekuwa na heading na kumbukumbu namba ingekuwa vema zaidi
ReplyDeleteKWA MARA YA KWANZA KTK HISTORIA YA TANZANIA, AKA BONGO LAND, BAADHI YA WABUNGE WANAHAHA NA KUOMBA WASICHAGULIWE KUWA MAWAZIRI, KWANI HAPA KAZI TU!
ReplyDeleteHAYO NDIYO MABADILIKO YA UKWELI, KWA KWELI NI VITENDO TU SIYO MANENO, KURA ZETU ZINATENDEWA HAKI. HONGERA SANA RAIS, TUNAKUOMBEA. WATAPIGANA NAWE LAKINI HAWATASHINDA MAANA MUNGU YUKO PAMOJA NAWE. AMINA
ReplyDeleteUFUATILIAJI NDIO TATIZO KUBWA NCHI HII LAKINI TUMEANZA VZRNA RAIS AMEONYESHA MFANO NA VIONGOZI WENGINE WAENDE TEMEKE NA MWANANYAMALA TUSIMNGOJE RAIS TU PEKE YAKE ATACHOKA. WAKUU WA MIKOA WILAYA HARUWASIKII!!!!!
ReplyDelete