Na Swahilivilla blog.  Washington D.C
Jana ililkuwa ni "Siku ya Maruhani" nchini Marekani. Siku hii ijulikanayo kama "Halloween" husherehekewa kila tarehe 31 Oktoba, na ina historia ndefu.
Siku ya Maruhani ilianzia huko barani Ulaya kiasi miaka 2,000 iliyopita ikifungamana na imani za kishirikina. Wazungu walipoyavamia mabara ya Amerika walihamia pia na utamaduni mila, desturi, dini, na silka zao - na sema upendavyo. Miongoni mwa hayo ilikuwa ndiyo hii siku ya Maruhani ambayo jina lake la asili ni "Samhein".
Sherehe za Maruhani  Photograph by treasuredragon/iStock.

Tuyaachie ya historia kwa wanahistoria, lakini kwa ufupi hii iliaminika kuwa ni siku ambayo pepo, majini, maruhani, mazimwi na mizimu au mizuka ya watu waliokufa hurejea hapa duniani katika maeneo yao ya asili na kujichanganya na watu waliohai.
Maudhui kuu ya siku hii ni kutisha, kuadhibu na mauti, ingawaje katika enzi zetu za leo imekuwa ni siku kuu ya watoto zaidi kuliko watu wazima. Sherehe zake hufanyika kuanzia familia, mitaa, makazini na hadi kufikia Ikulu yenyewe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mashetani sio maruhani ni vitu tofauti ,,,,

    ReplyDelete
  2. HUO NI UONGO ULIOPITILIZA NA UZANDIKI WA HALI YA JUU,HALLOWEEN NI SIKUKUU YA MAVAZI(CUSTOME).SIO SIKUKUU YA MASHETANI,KWA HIYO KILA MTU ANAVAA VAZI ALIPENDALO NDIO MAANA KUNA WENGINE WANAVAA KAMA FARAO,DAKTARI, FIREMAN,NURSE NA HATA WAPISHI WAKUU(CHEF). SASA KUSEMA NI SIKUKUU YA MASHETANI HUO NI UONGO AMBAO UNAPOTOSHA MAANA YA HALISI YA HALLOWEEN.

    ReplyDelete

  3. Kwa muono wangu mimi, vitu vilivyoko madukani vinavyohusishwa na sherehe za halloween na namna ambavyo asilimia kubwa ya watu wanaosherekea wanavaa, inahusiana zaidi ma-skeleton, mafuvu na vingine vingi vya kutisha vinavyofanana na hivyo. Pia mara nyingi kuna alama fulani inatumika, inachukuliwa aina fulani ya boga, wanalitoboa linakuwa na macho na mdomo halafu wanaweka design fulani ya mshumaa unaowaka ndani ya hilo boga, kwa hiyo,picha inayoonekana ni kama kichwa cha mtu ambacho moto unatoka machoni na mdomoni. Yaani mpaka hapo,taswira inayoonekana ni ya ulimwengu wa giza. Kama kuna namna nyingine ambayo watu wanavaa tofauti na vitu vya kutisha, basi ni katika kuifanya tu sherehe hiyo ionekane ya kawaida. Lakini kiukweli NI SHEREHE ZA ULIMWENGU WA GIZA. Mungu Atufungue macho tuone kiroho mambo yanayoendelea hapa duniani. Tena Atusaidie tuwalee watoto wetu katika njia ya Mungu,

    ReplyDelete
  4. Kama huelewi Halloween ni sikukuu ya mashetani,basis ni vizuri ukatafuta,investigate kuliko kubisha kitu usichokijua.Halloween si sikukuu ya costumes kama ujuavyo wewe.

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na mchangiaji wa tatu hapo juu, tena hata kwenye part zao za kusherehekea Haloween day, sometimes kwa wengine unakuta na 'dress code' ni za ki Haloween haloween tu, almuradi watu wafurahi na kuisherehekea siku hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...