Mwandishi wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi, Airtel kupitia huduma yao ya
kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap wanakuletea punguzo la bei
za tiketi za kumshuhudia staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond
Platnumz, Krimasi (kesho) ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem
jijini Dar.
Akizungumza na Amani, Meneja Huduma wa Airtel, Moses James
alisema kuwa mteja anatakiwa kununua laini yake ya Airtel kisha kujiunga
na huduma ya Airtel Money Tap Tap na baada ya hapo atakabidhiwa namba
ya siri ambapo ili kuanza kutumia huduma hiyo rasmi ni lazima mteja
aweke kiasi cha kuanzia shilingi 11,000.
“Watoa
huduma wetu wa Airtel wanatoa huduma hii katika matawi yetu yote na
hata ukienda Dar Live utaipata. Siku ya shoo ya Krismasi unachotakiwa ni
kuonesha kadi yako ya Airtel Money Tap Tap kisha utapunguziwa bei ya
tiketi kuanzia VIP ambayo ni 30,000 utapata kwa 25,000, kawaida 15,000
utapata kwa 10,000,” alisema Moses.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...