Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso,akifatiwa na Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Airtel Fursa msimu wa pili. Akishuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2. mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24
kupata fursa za kuinua biashara zao, uliyozinduliwa Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24  kupata fursa za kuinua
biashara zao. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Kijana aliyewezesha kupitia mradi wa Airtel FURSA msimu wa 1, Mohamed Kigumi akipongezwa na  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso kwa kufanya vizuri katika biashara yake wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mradi wa Airtel FURSA , mradi wenye lengo la kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kukuza biashara zao. Wakishuhudia (kushoto) ni Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya. (kulia) ni Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula
 Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili
 Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifatilia uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Saalam
Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akiteta jambo na  Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili.
 

  *   zaidi ya shilingi billion 1 kusaidia  miradi ya kuwawezehsha vijana llings
 Kampuni ya simu ya mkononi
ya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha
vijana ujulikanao kama "Airtel FURSA" kwa lengo kuendelea kudhihirisha
kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini
Mradi wa "Airtel FURSA" ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la
kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa
vitakavyowawezesha kukuza biashara zao

Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA"  umewawezesha vijana zaidi ya 2500
wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na
wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea
vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa
zaidi kwa jamii inayowazunguka.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil
Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake  kuwawezesha vijana na
kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania
" Mradi huu wa "Airtel FURSA"   unadhihirisha dhamira yetu ya
kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na
kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA" umetoa matokeo
mazuri sana na  tumefanikiwa  kugusa maisha ya  maelfu ya vijana wengi
kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,"

"Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani  shilingi  billion moja
ili  kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa
na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada
ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za
mkononi" alisema Colaso.

Akizindua rasmi mradi wa "Airtel FURSA" Naibu waziri  Wizara ya Kazi
Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha  na
kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia
fursa hii ili kuboresha maisha yao. alisema Mh Mavunde
"Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali,
zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya
"Airtel FURSA" ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza
wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia
fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:"

"Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na
kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea
vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza  uchumi
wa nchi" aliongeza Mavunde

"Airtel FURSA"  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa
kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia
mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi
kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya
biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma
maombi yako kwa kupitia barua pepe ya
airtelfursa@tz.airtel.com<
mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. Or
tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com<http://www.airtel.com>  na
ujaze fomu yako ya maombi
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...