Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta akikabidhiwa baadhi ya zawadi mbalimbali na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.
Leo tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg.
Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar
Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es
Salaam.
Mufti Mkuu mbali na kumpatia
zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia
alipata nafasi ya kumuombea dua ya mafanikio zaidi huko aendako
Ulaya na kumpa nasaha asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati
na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi.
Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye.
Kila lijalo ni rizki ya Mola. Mbwana,umetuonesha njia bora ktk kuboresha imani, utanakuwa na mafanikio makubwa. Katika hili na jingine Mbwana dumisha imani yako na juhudi katika shughuli zako na kazi yako. Tunakutakia kila la kheri ktk mkataba wako mpya. Utakutana na changamoto mabalimbali katika safari hii ya maisha. Hizo ni kawaida,utayashinda yote na kufanikiwa zaidi, tuliza roho,ongeza bidii na ushirikiano. Katika hili umeonesha mfano mzuri wa kuigwa. La mwisho kutoka kwangu ni hili. Popote uendapo jitambue wewe na dini yako, Wazazi na ndugu zako, heshimu Serikali iliyopo na usiingilie familia za watu. Hii ni siri ya mafanikio. Kheir In Shaa Allah
ReplyDeleteMrs. B. Sam, Kanyamahela, Kibondo