BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kwa utekelezaji wake wa majukumu yake kwa jamii.
Basata walieleza hayo baada ya kufanikisha kibali cha Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza kufanyika Machi 26-28 hapa nchini.
Kwa Mujibu wa Katibu Mtendaji Godfrey Mungereza, Msama ameliandaa tamasha hilo kufanikisha waimbaji wa injili kupanda jukwaa moja bila kuchagua imani kwa kuamrishana mema.
Mungereza alisema, waimbaji wa muziki wa injili wanabadilishana uzoefu hasa na waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambako muziki huo unapiga hatua kimataifa.
Mungereza alisema kupitia tamasha hilo kutambulika zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania hiyo ni ishara ya kuendelea kufahamiana zaidi.
Aidha Mungereza alisema Tamasha la Pasaka linaiweka Tanzania katika sura ya kimataifa zaid i jambo ambalo ni la msingi kwa serikali.
Aliongeza kuwa jamii inapata mafunzo mbalimbali kwani jamii kwani waimbaji na jamii wanaunganisha uelewa kupitia tamasha hilo.
Sambamba na hayo Mungereza alisema Tamasha la Pasaka ni sehemu ya jamii hasa katika uwakilishaji wa pato linalotokana na viingilio vya tamasha hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...