Jumuiya ya wanarugambwa (Rugambwa Girls Foundation) wanayo furaha kukualika kwenye mkutano wa pamoja utakaofanyika tarehe 23 Januari, 2016 kuanzia saa 7 mchana, Leaders Club, Dar es Salaam.
Ukiwa kama mdau wa Rugambwa Sekondari: mwanafunzi, mwalimu, mtumishi wa aina yoyote aliyewahi kupita Rugambwa Sekondari pamoja wanafunzi wote waliosoma shule rafiki za Rugambwa (Ihungo, Kahororo, Bukoba Sekondari, Nyakato, Ntugamo Seminari, n.k. tunakualika kushiriki.
Lengo ni kukutana kubadilishana mawazo na kupeana mikakati jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha jubilee ya miaka 50 ya Rugambwa Sekondari itakayofanyika, Machi 2016 pamoja na ukarabati na uboreshaji wa shule hiyo.
Atakayesikia au kusoma tangazo hili amfahamishe na mwingine.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rugambwa Girls Foundation

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kumbe mpo? Tumieni fursa hii kurudisha fadhila na sifa kwenye shule yenu maana.........!

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, naomba unisaidie kuweka swali langu.

    Kulikuwa na shule iliyokuwa ikiitwa MWADUI SEKONDARI, na ilitoa wanafunzi wengi sana ninaowafahamu. Kwa bahati mbaya sijawahi kuisikia ikijadiliwa wa watu waliosoma huko, je hii shule bado ipo inaendelea, au iliishafungwa? Kama ipo hao watu wote waliopitia huko hawaoni wivu kuisadia shule yao, kama wanavyofanya wengine? Akina Rugambwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...